Elimu ya mahaba

simulizi za kusisimua

KILA DEMU NA UTAMU WAKE

Watu waliomjua tangu akiwa na umri wa miaka 17 walidhani huenda ni umri unaomsumbua. Wakaamini kwamba atakapokuwa mtu mzima angeacha, haikuwa hivyo kwani kila siku, Boi ambaye jina lake halisi ni Lawrence Godfrey aliwabadili wanawake wa kila rika kama daladala zinavyopishana barabarani.
Mwanamke gani amtongoze na kumkosa? Sketi gani nzuri ipite mbele yake bila kuingia mikononi mwake? Jambo hili liliwafanya rafiki zake wajue kabisa huenda Boi anatumia dawa za kuwatia kiwewe wanawake wazidi kumpenda.
Kila rangi ya mwanamke, mwenye sifa za uzuri, Boi aliweza kumgusa na kuona mwisho wa raha zake.
Katika daftari lake la kumbukumbu za wasichana aliotembea nalo lilijaa, jambo ambalo lilimtisha sana rafiki yake aitwaye Dullah!
“Kaka, hivi unatumia kinga?” Dullah akavunja ukimya.
“Natumia kaka, kwani umeshawahi kusikia nina mtoto sehemu?”
“Hapana, ila punguza bwana…”
“Najaribu kupunguza nashindwa, wanawake wanatofautiana sana, ukikutana na huyu anaguna, mwingine analia, mwingine anacheka, mwingine ananyamaza kimya. Nakuambia ukweli, yupo mwingine anapiga kelele hadi mtaa wa tatu wanasikia.Tangu nimewajua, nimegundua wako tofauti kuliko watu wanavyofikiri…”
“Hapo napo kweli, lakini unawajuaje?”
“Kuwajua ni hapo unapokuwa nao kitandani…”
“Duh! Unajua sielewi kabisa.”
“Poa, hunielewi acha nikueleweshe.Ngoja nikuulize swali.”
“Uliza.” Dullah akadakia, akitega sikio vema.
“Hivi, sikio langu na lako lipo sawa?” Boi akamuuliza Dullah.
“Hapana, sikio langu refu kidogo na limepinda kama sikio la Popo, lakini lako dogo na limesimama kama la sungura…”
“Mmmh! Hata wanawake katika maumbo yao yametofautiana, mimi na wewe ni wanaume lakini tupo tofauti, unalijua hilo?”
“Nafahamu!”
“Mimi huenda Boi mkubwa kuliko Dullah!”
“Kabisa!”
Wakati wanajadili suala la mademu kutofautiana, simu ya Boi ikaanza kuita, akaitazama na kuachia tabasamu pana lililoshiba midomoni mwake.Hawakuwa sehemu nyingine isipokuwa chumbani kwa Boi wakipeana darasa la mahaba.
Getho la Boi lilikuwa maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam karibu kabisa na Hospitali moja binafsi. Boi ni mwanafunzi mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akiwa anasomea biashara. Dullah naye ni mwanafunzi wa chuo hicho hicho, mwaka wa pili. Ajabu ni kwamba pamoja na Dullah kumzidi daraja la elimu, Boi ndiye aliyefahamika zaidi kutokana na tabia yake ya kupenda na kupendwa na wanawake.
Simu iliendelea kuita, na wakati huu Boi aliwaza jibu gani ampe msichana huyo, siku hiyo alishawaahidi wasichana wawili na wote alipanga kulala nao kwa zamu. Matha hakuwa kwenye ratiba kabisa ya siku hiyo.
“Sikiliza, anapiga Maimatha…,” Boi alimbonyeza Dullah!
“Matha, huyu wa IFM!”
“Haswaa, sijui ni mwambie vipi, maana hapa nimeshaongea na Janeth, anakuja getho ili nimpe dawa.”
“Dawa gani?” Dullah alitaharuki, inamaana Boi ameshakuwa daktari?
“Hujui kuwa Janeth amesema anajisikia mgongo unamuuma sana, hivyo lazima nimnyooshe kidogo na kumpa dozi murua?” Alipotoa kauli hiyo, Dullah akacheka sana.

“Hivi unawezaje kutembea na wasichana wengi kiasi hicho bila kuwagonganisha?”
“Akili kaka, naenda na muda na uongo wangu kamwe sisahau. Pamoja na kuwa bingwa wa kuwachanganya, sitasahau gemu moja gumu. Siku moja nilikuwa na kiu sana, nikamuita Naomi aje saa nne ili saa sita nimuondoe na kumleta mwingine. Nikapanga miadi na Leila yule mtoto wa kigogo wa Bandari kuwa aje saa nane, kwasababu niliamini huenda wasingefika na ningekosa nikaongea na Mei kuwa siku hiyo ningelala naye getho kwangu.



Ajabu nilishapanga tena mechi na Richael, huyu dada ana duka la nguo Kariakoo mtaa wa Kongo kuwa usiku ningekutana naye anipe mautamu kabla ya kulala na Mei.
Sasa kwa bahati mbaya wote wakaja kwa wakati uliokaribiana sana na hapo ndipo balaa. Naomi alifika saa saba na nusu, na Leila anakaja saa nane, Mei naye aliwahi akidai anatamani tuwe pamoja kuanzia mchana hadi usiku, bila kunipigia simu akatia timu. Unaambiwa niliwapanga na kupiga chenga za Messi, kwanza aliyechelewa alipokaribia kufika akanipigia nikamwambia nimetoka kidogo baada ya kumsubiri sana, nikamtaka anisubiri baa ya jirani…ilibidi afanye hivyo. Leila aliyeenda na ‘time’ ikabidi nianze kumshughulikia haraka sana…waaaacha kabiiiisaa!”
“Uligawa vipi muda?”
“Sikiliza, simu yangu kwanza haina sauti na hata ninapokuwa na mwingine sipokei kabisa na kama niliamua kupokea basi niliongea kwa mafumbo kiasi cha kutoshtukiwa kama naongea na mwanamke…”
“Ehee…”
“Baada ya kucheza mechi ya muda mfupi na kuhakikisha kwamba wote tumefunga bao, nilimwacha na kwenda kwa mwingine na yule kumtelekeza chumbani.”
“Baadaye niligundua nimezidiwa na ili niwaweze, nikampigia rafiki yangu Frank kuwa amtulize hotelini nakuja, unaambiwa niliwapanga kama nyanya sokoni na kila mtu alipata dawa.”
“Dah! Boi, punguza bwana…”
“Nishakuambia, sijui ni laana au vipi, kila siku watoto wazuri wanazaliwa, na wote ni wazuri kuliko wa jana…”
“Mikorogo tu hiyo kaka,” Dullah akashusha pumzi baada ya kuwaponda.

kila demu na utamu wake

kila demu na utamu wake
... kila demu na utamu wake..

mara...

Simu ya Maimatha ilipokelewa, tena bila wasiwasi, Boi akamwambia kuwa amelimisi sana penzi lake.
“Weka loudspeaker!” Dullah alimnong’oneza sikioni Boi.
“Yaani, Boi…sijui nisemeje, nakupenda sana na juzi ulinichanganya, kila nikikumbuka naona heri nikuone…”
“Darasani leo umeingia?” Boi akauliza, hakutaka kukutana na mrembo huyo, alikuwa na miadi na Janeth, hivyo aliogopa kufumaniwa.
“Nimeingia kipindi cha asubuhi tu, dear…uko wapi?”
“Nipo maeneo ya Mwenge ila nataka kwenda Sinza.”
“Basi, nisubiri hapo kwako,” Maimatha alisema kwa sauti ya chini iliyojaa pumzi za mahaba.
“Nipo na Dullah, tumepitia saluni kunyoa,” Boi alitania akimbonyeza Dullah.
“Unanyoa nini?”
“Ndevu…”
“Hapana dear, usinyoe…nazipenda sana ndevu zako my darling. Mbona unataka kunitesa?”
“Acha nizinyoe washikaji wananicheka sana wananiita Osama, wengine kidevu.”
“Sikiliza Boi, usinyoe nitakupa elfu hamsini, kweli.”
“Sawa, unakuja?”
“Sasa hivi, nataka leo unipe mapenzi ya juzi, umesikia D wangu…”
“Ndiyo, nitakupandisha nitakushusha, utafurahi…,”
“Sawa, ngoja nikaache gari langu likiendelea kuoshwa kisha naja,” alisema Maimatha kwa sauti iliyojaa michujo ya mahaba. Sifa za mrembo huyu, alikuwa mrefu na mnene kiasi aliyebarikiwa wowowo la nguvu ambalo liliwacha wanaume wengi vinywa wazi alipopita mbele yao.

... inaendelea ndani ...

kilademu na utamu wake

kilademu na utamu wake
... na utamu wake..

Jumanne, 26 Agosti 2014

MAFIA WA BONGO (1)
Mwandishi, Zubagy Akilimia, 0712313191

Ukimuona kwa jinsi alivyo unaweza kusema si Mtanzania halisi, hii ilitokana na urefu wake  wa futi saba kasoro na weusi uliopitiliza. Kwa kumtazama ungeweza kusema ni Mkikuyu kutoka Kenya au rai wa nchi jirani ya Rwanda. Pamoja na kwamba alikuwa na umri wa miaka 17, ungemkisia kwa kusema ana miaka 30. Umbo lake liliweza kutisha wanaume wengi wavimba mbavu mbili na kuwavutia wasichana wenye kupenda mwanaume mwenye mwili mkubwa.
Kijana huyu jitu la miraba mnne alizaliwa Tarime vijijini na kukulia huko huko Mkoani Musoma.
Wakati anazaliwa alikuwa na kilo gramu nne na nusu(kg 4.5).Mtoto huyu kwanza alichelewa sana kutembea na hata kuongea, wazazi wake awali walidhani wamepata mtoto bubu na mlemavu, haikuwa hivyo kwani baadaye akiwa na miaka miwili aliweza kutembea na kuongea vizuri Kikuria.
Utaalamu wake mkubwa, ni kupiga shabaha na ujuzi wa kuzaliwa nao ulikuwa kukarabati bunduki aina ya ‘Gobole’ na Bastola aina zote na hata ‘Machine Gun’.
Watu wengi wanafahamu wazi watu wanaoweza kutengeneza au kukarabati bunduki mara nyingi ni waliopitia mafunzo wa kijeshi, kwa upande wa Masato Lwegambura watakuwa wamekosea.
Kijana huyu si miongoni mwa watu waliopitia jeshi, ingawa alitisha na kuonekana zaidi ya mtu aliyepitia mafunzo ya jeshi. Huu ni uwezo binafsi uliowashangaza hata askari waliokuwa wakimtafuta kwa ajili ya kumtia mikononi mwa polisi.
Wengi walihisi huenda anatumia dawa za kichawi, kutokana na uwezo wake wa kuua na kutokomea bila kukamatwa.
Unaweza kujiuliza kichwani mwako.Je, huyu kijana mdogo ameweza kupata wapi ujuzi wa kukarabati, kutengeneza silaha na kuzitumia, sasa ukakuna kichwa na kuguna. Mhh!.
Ukweli, historia ya Masato ni nzito sana, ni kijana aliyelelewa na babu yake mzee Simon Lwegambura, baada ya baba na mama yake kuvamiwa na kuuawa na wananchi wenye hasira kali kwa kuchoshwa na ujambazi wa baba yake. Kifo hicho ndicho kilichosababisha Masato kuwa yatima na kutowafahamu wazazi wake. Babu yake alimchukua mjukuu huyu na kwenda naye kijiji cha mbali na mjini, awali familia ya Lwegambura ilikuwa ikiishi Musoma mjini maeneo ya Mwembeni. Masato akiwa na umri wa miaka mitatu aliishi kiseja na babu yake ambaye hakuwa na mke wala mtu mwingine wa kumsaidia. Aliishi na Masato akimpikia uji, maziwa ya Ng’ombe maana alikuwa mfugaji mkubwa wa Ng’ombe.
Kutokana na ukorofi wa mzee Simon Lwegambura, hakuna jirani aliyekuwa anamsogelea, mara nyingi marafiki zake walikuwa viongozi wa nchi jirani na matajiri ambao walifika nyumbani kwake asubuhi sana au usiku wakiwa na magari.
Hakuna aliyeelewa mzee Simon alikuwa akifanya biashara gani na viongozi na matajiri hao. Kuna watu walianza kusema huenda mzee Simon ni mpelelezi maana hata magari ya vigogo yalifika kwake na kuondoka. Tetesi zikaenea mtaani, na kumfanya Mzee Simon aigopwe sana kijijini kwao. Wageni mbalimbali ambao hawakujulikana walikotoka walifika na kuondoka kisha kurudi tena na kilichowashangaza wengi ni ile hali ya mgeni kuwa lazima akienda arudi tena.
Kilichomsaidia watu wengi kushindwa kumuelewa kazi halisi ya Mzee Simon, ni kule kutopenda kuzoeana na hata wazee wenzake. Zaidi ya salamu, hakuna mazungumzo mengine.
Ufinyu wa kutozoeana ukazidi kuwatia watu wasiwasi, wengine walimuona huenda ana uwendawazimu kama si laana.
“Haiwezekani mnaishi na mtu hata hana mazoea wala haendi kwa mtu, yeye rafiki zake ni wageni…” Mzee mmoja alilalamika, akajaribu kujipendekeza akachoka maana mzee Simon hakutaka mazoea.
Rafiki yake mkubwa mzee Simon ni mjukuu wake, hata alipoanza shule ya msingi, majirani na watu mbalimbali walianza kumchunguza Masato na kutaka kujua ukweli wanavyoishi na babu yake.
“Masato, nyumbani nani anakupikia chakula?”
“Chakula, tunapika na babu…”
“Ahaa! Kwa hiyo hakuna mtu anayeishi na ninyi?”
“Hakuna tupo wawili tu…”
“Safi sana, na wale wageni wanaokuja na kuondoka wanaleta nini au wanakuja kuchukua nini?” Huyu alikuwa ni mjumbe wa nyumba kumi aliamua kumfuatilia Masato shuleni.
“Hakuna kitu, wale ni ndugu zetu…”
“Ahaa, mbona wanakuja na kuondoka hawalali?”
“Hakuna nafasi ya kulala, sisi tuna vitanda viwili tu…”
“Sawa, babu yako anafanya kazi gani ndani?”
“Hana kazi, anapenda kusuka ukili tu…” Masato alidanganya, kumbe mzee huyu ambaye ni mjumbe hakujua kama Masato alishapewa elimu na babu yake kuhusiana na watu watakaotaka kumpeleleza.
Akili yake ilishalifahamu hilo mapema ndiyo maana alimfundisha maisha ya ukubwa na jinsi ya kujibu maswali na hata kujitetea.
Baada ya kupeleleza huo wa muda wa dakika kumi, hatimaye Masato alienda shuleni na kuingia darasani. Hata hivyo, pamoja na kuwa darasani akimsikiliza mwalimu kwa makini, somo la babu yake ndilo alilolipenda zaidi kuliko la darasani.
Akiwa na umri wa miaka kumi na moja, darasa la tano Masato alishafahamu kusafisha bunduki maarufu kwa jina la ‘Gobole’, Bastola za kila aina, mfano Revolver, M92 Beretta, Short Machine Gun(SMG) nk. Alipofikisha umri wa miaka 13, babu yake ambaye kazi yake kubwa ilikuwa kukarabati na kutegeneza silaha kwa siri bila jeshi la polisi kufahamu, alimfundisha ufundi wa kukarabati silaha zote.
Kutokana na kuipenda kazi hiyo na kupenda kutumia bastola, Masato akawa mtaalam na hata zilipoletwa bastola za kusafisha na kutengeneza aliweza kuifanya kazi hiyo kwa ubora wa hali ya juu. Babu yake alishangaa sana na upendo kwa mjukuu wake ukaongezeka maradufu. Akili mwake, alifahamu amepata mrithi wa kazi yake, jambo lililompa faraja.
“Umesikia mjukuu wangu, hii ni kazi ninayoifanya kwa magendo, sipendi mtu yoyote ajue zaidi ya wateja wangu,” ilikuwa sauti ndogo huku akimshika kichwa na kuchezea nywele zake.
“Nimekuelewa babu, na ukweli babu hii kazi naipenda sana.”
“Nashukuru kusikia hivyo. Ila nakuonya…usije kuiga kazi ya baba yako…”
“Kazi gani?” Masato akamwangalia babu yake kwa udadisi. Hakujua kama baba yake alikuwa jambazi sugu na Mafia wa Bongo.
“Baba yako alikuwa jambazi hatari sana Tanzania hii, nilipenda awe mwanajeshi kwa ajili ya kutetea rai na aridhi yetu ya Tanzania, kumbe alipokwenda jeshi alienda kwa nia ya kujifunza uwezo wa kuua, kutumia silaha za kivita na ufundi mwingine wa shabaha…”
“Dah! Baba yangu alikuwa Mafia! Kama akina Van Damme, Bruce Lee?”
“Zaidi, kwani Van Damme na Bruce Lee walikuwa wanaigiza filamu tu…yeye alikuwa anafanya kweli, akisema naua leo lazima aue kweli, akisema navamia duka na kupora pesa lazima afanye hivyo,” yale mazungumzo yalimvutia sana Masato bila mzee Simon kuelewa kuwa alikuwa anamharibu mjukuu ubongo wake. Alipenda sana kutumia bastola kuliko kiumbe yoyote duniani.
Kadri siku zilivyozidi kwenda, umri wa babu ulizidi kumtupa, kazi nyingi zilikuwa zinafanywa na Masato. Kitu kikubwa ambacho kiliwashangaza majambazi wengi, ni ile hali ya shabaha na uelewa wa kutengeneza bunduki kwa kutumia miti na vyuma.
Kuna wakati majambazi wa Mwanza wa Kundi la Jembe walifika Tarime kwa ajili ya kumuomba Masato aweze kujumuika nao. Kijana huyu aligoma kabisa, maana alipewa historia ya kifo cha baba yake.
Hata hivyo, alipenda sana kutumia bastola na ataitumia wapi, kama siyo kwenye matukio ya ujambazi? Hili lilikuwa ni zoezi gumu sana kwake.
“Babu, naomba unifundishe ujuzi mwingine maana naona wewe sasa hivi umezeheka sana…” Masato akiwa na miaka 17 alimweleza babu yake.
“Kitu ambacho nimekuwa sijakufundisha ni kutengeneza baruti na mabomu ya kutupa kwa mkono, na itabidi ufahamu vitu vya kutengenezea na adhari zake kabla ya kuanza zoezi. Itabidi twende msituni ili kunifundishe zaidi,” Babu mtu alimwambia mjukuu wake, alishaelewa kuwa siku yoyote anaweza kuaga dunia.
Huu ni mwanzo tu, hadithi ndiyo kwanza inaanza. Fuatilia ujue Masato amefanya mambo gani? Usikose kusoma kitabu changu cha WANAWAKE WAZURI MATESO, kinauzwa TSH 4000/=  Kwa wauzaji wa magazeti nchi nzima.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni