MKASA WA KWELI
NYUMBA NDOGO ILIVYOVUNJA NDOA YANGU (1)
Kilikuwa chumba kidogo chenye vikirokoro vingi
vya vyombo, viatu, kabati la nguo, jiko, mafurushi ya nguo na meza ya chakula.
Chumba hiki kilimilikiwa na Willbroad
Masumbuko, aliyekuwa akiishi na mkewe aitwaye Vumilia. Ukweli, si kwamba
mwanaume huyu alishindwa kujenga nyumba, lahashaa. Kazi yake ilikuwa
ikimuingizia kipato kikubwa sana cha kuweza kuwa na hata vyumba viwili, sema
aliegemea upande wa ulevi na wanawake wengine.
Kazi yake ya udereva wa malori yaliyokuwa
yakifanya safari zake za Congo, Zambia, Malawi, Uganda na Zimbabwe ilimfanya
apate pesa nyingi. Willbroad hakuwa na huruma, usiku mzima alikuwa akisumbuana
na mkewe, kwa kumtaka mapenzi.
Vumilia alikuwa akihangaika, tumbo la uzazi
lilikuwa likimkata si kidogo. Maumivu ya uchungu yalimfanya alie sana, lakini
mumewe hakujali kama mkewe ujauzito wake ulikuwa umefika muda wa kujifungua,
siku hii alichokuwa akitaka ni mapenzi tu.
“Vumilia, huwezi kuninyima mapenzi, nipe
nitanue njia…nimekaa Congo mwezi mzima, ulikuwa na mwanaume gani unayempa
mapenzi?”
“Sina mwanaume mume wangu, sijawahi kufikiria
kukusaliti…nionee huruma siwezi kukupa penzi kwa sasa mume wangu, tumbo
linaniuma sana…”
“Linakuumaje ? Acha utani, nipe mapenzi…”
Willbroad aliendelea kutumia nguvu ili kupata penzi.
“Utaniua mume wangu, usinibake…tutamuua mtoto
wetu…” Vumilia alijaribu kumzuia mumewe asiweze kumbaka, ikashindikana.
Willbroad Masumbuko, mwenye nguvu nyingi aliendelea kumng’an’gania mkewe ili
amalize haja zake. Hakufikiria maumivu aliyokuwa akipata mkewe, hakujali kwamba
mkewe anasumbuliwa na uchungu wa uzazi aliendelea kumtanua miguu na kuingia
katikati ya miguu akijiandaa kumuingilia kimwili.
“Mume wangu, nionee huruma, utaniua
bure…vumilia nikijifungua nitakupa tu, kwanini unaning’ang’aniza mapenzi…”
“Sasa unafikiri nilikuoa ili ufanyeje? Ndoa
imekushinda?”
“Haijanishinda, uliza hata wanaume wenzako.
Mwanamke akiwa mjamzito anayetakiwa kujifungua leo anafanywaje? Ungekuwa na
somo juu ya uzazi ungenionea huruma, natamani nikuhamishie maumivu ya uchungu,
hakika ungeniacha…najua umenioa ili nikutunze, nivumilie, naumia mume
wangu...tumbo linauma…,” alisema maneno hayo Vumilia akizidi kuangua kilio.
Mumewe aliyekuwa na roho ya kinyama, hakujali sauti wala kilio chake . Maungoni
alisisimka kweli kweli na hapo ndipo akamalizia kufungua kufuli na kuanza
kumuingilia mkewe wakati anasumbuliwa na uchungu wa uzazi. Mfuko wa uzazi
(chupa) lilishapasuka na hali ilikuwa ni ngumu sana kwa Vumilia kuweza
kuvumilia.
“Naona umeamua kuniua mume wangu…”
“Sikuui, uliitaka ndoa..acha unipe haki
zangu…”
“Najua ni haki zako, ila huna huruma…huna
uvumilivu wa ndoa…kama ndoa zote zipo hivyo basi, itabidi niombe talaka…”
“Talaka sitoi, sijui kuacha, najua
kuoa…tulia…,” alipoona ugomvi umezidi, Vumilia akaanza kuangua kilio kwa sauti
ya juu, mumewe akamnasa kibao cha shavuni, akanyamaza kidogo huku machozi
yakimtirirka mashavuni na milio ya kwikwi ikasikika.
“Niue tu…unizike…,” alisema Vumilia kwa tabu,
huku jasho likimtoka mwili mzima.
Katika kufanyiwa ukatili huo, alijikuta
akihisi kuishiwa nguvu. Mumewe hakujali, aliendelea kumuingilia kimwili hadi
alipomaliza haja zake na kumuacha amelala hoi kitandani.
“Pole sana, sasa ngoja niende kazini, kuna
kontena naenda kupakia kisha nirudi Congo…nitakuja jioni kujua
unaendeleaje…”Willbroad Masumbuko alisema na kumwachia mkewe shilingi elfu tano
za matumizi ya siku hiyo.
“Mume wangu, sina pesa nyingine…hizo hazitoshi
kwenda hospitalini, si unajua hali yangu jamani…”
“Hazikutoshi, unataka kiasi gani?”
“Yoyote inayofaa, hata elfu ishirini, hivi
unajua hata vifaa vya kujifungulia sijanunua…”
“Kwani vinauzwa, si unaenda kujifungua
hospitali za serikali?”
“Ndiyo, lazima niwe na vifaa….kama pamba,
gloves na pesa zingine za dawa…”
“Wewe nenda, utanipigia simu…” alijibu
Masumbuko na kutoka.
Alimuacha mkewe aliendelea kuangua kilio,
juhudi za kuomba aongezewe pesa ziligoma. Afanyaje?
Dakika moja baadaye, Willbroad alirejea,
“Nimesahau, naomba uniazime simu yako…”
“Mume wangu simu hii nitaitumia kwa
mawasiliano, hali yangu si nzuri, nataka niwapigie ndugu zangu…”
“Wewe nipe nitawapigia…” aliichukua simu ya
mkwe na kutoka.
Bila huruma, Masumbuko aliondoka zake na
kurudishia mlango.
*****
Vumilia alishindwa kujizuia, uchungu uliendelea
kumsumbua, ukizingatia walikuwa wakiishi Mwananyamala A, nyumba ya kupanga.
Alipoona hana msaada, alijaribu kuinuka kitandani kwa tabu sana huku amebana
miguu ili mtoto asiweze kutoka. Haja kubwa ilikuwa inamsumbua, lakini akahisi
akiingia msalani mtoto angeweza kutumbukia chooni.
Alitembea kwa kushikilia ukuta hadi kufanikiwa
kutoka nje.
“Jamani nikoeni, nakufa sasa…”
“Vumilia, una tatizo gani?”
“Uchungu, naomba mnipeleke hospitali, mtoto
anataka kutoka…”
“Basi, ngoja tutafute usafiri…” Mama Amina,
jirani wa Vumilia alisema, alitoka akikimbia hadi kituo cha teksi, akaongea na
dereva teksi kwa ajili ya kumuwahisha mwanamke huyo hospitali.
“Mumewe yupo wapi?” dereva teksi alisema.
“Kandoka, yaani mwanaume hamjali mkewe ni hawa
madereva wa malori, sijui ni mtu wa aina gani?”
“Mpumbavu sana, sasa kwanini alimuoa?”
“Hata sijui, mwanaume mwenyewe katili kweli,”
alisema Mama Amina.
Walipofika nyumbani kwa Vumilia, waliegesha
gari nje na kumchukua wakamuwahisha hospitalini ya Mwananyamala, walimpokea na kuwambia
itabidi apelekwe Muhimbili.
*****
Chumba cha upasuaji hospitali ya Taifa
Muhimbili, kulikuwa na wanawake kumi waliokuwa akijifungua wakati huo. Mmoja wa
wazazi waliokuwa wakijitahidi kusukuma mtoto alikuwa Vumilia Jorome. Jasho
lilizidi kumtoka huku akihangaika na madaktari wakijaribu kumsaidia ingawa
ilishindikana.
“Kwanza, mbona kuna mbegu za kiume humu…”
“Mume wangu alikuwa akinilazimisha mapenzi…”
“Mpumbavu sana. Yupo wapi?”
“Hayupo, ameondoka na kunitelekeza…”
“Kweli, ni mumeo au hawara…”
“Mume wangu…” Vumilia alizidi kuangua kilio cha
uchungu.
“Mtoto amekaa vibaya, sasa ili kuweza kuokoa
uhai wake na mtoto itabidi ufanyiwe upasuaji haraka iwezekanavyo…” Dokta Kim
alimweleza daktari mwenzake.
“Ni kweli, maana hata hivyo njia ya binti
huyu ni ndogo…”
“Kweli, itabidi afanyiwe upasuaji…”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni